Huduma ya reli nchini India husafirisha mamilioni ya watu ndani ya nchi. Na sasa wanaishukuru optic fiber kwa kupeleka mtandao wa internet kila kona ya nchi.
Saturday, May 6, 2017
Jinsi mtandao wa bure wa Wi- fi unavyoleta mabadiliko chanya kwenye stesheni za treni India
Huduma ya reli nchini India husafirisha mamilioni ya watu ndani ya nchi. Na sasa wanaishukuru optic fiber kwa kupeleka mtandao wa internet kila kona ya nchi.
Monday, December 5, 2016
Je unajua simu yako ya Android inaweza fanya kazi kama remote control kwenye kifaa chochote kile bila kujali aina ya kifaa (TV,AC, Satellite na DVR).
Je umepoteza remote ya TV,AC, Satellite na DVR ? tumia (IR Blaster
Sensor) kwenye simu yako ya Android nautaweza kutumia kama remote bila
kuwa na haja ya kuangaika madukani wala kujali Brand ya kifaa. Fata
hatua hizi.

Kuna aina nyingi sana za TV, AC, Satellite na DVR katika matumizi yetu ya kilasiku.
Maranyingi imekuwa kazi ngumu sana kupata remote control ya kifaa chako pale inapo potea au kuharibika pia ningumu sana kukuta remote moja unaweza kuitumia kwenye vifaa vyako vyote nyumbani bila kujali aina ya kifaa hicho.
Kama wewe nimtumiaji wa simu ya Android ingia Google Play na upakue App hii na uanze furahia kutumia simu yako kama remote kwa vifaa vyako vyote ndani ya nyumba yako.
Pakua hapa : IR Universal Remote

Kuna aina nyingi sana za TV, AC, Satellite na DVR katika matumizi yetu ya kilasiku.
Maranyingi imekuwa kazi ngumu sana kupata remote control ya kifaa chako pale inapo potea au kuharibika pia ningumu sana kukuta remote moja unaweza kuitumia kwenye vifaa vyako vyote nyumbani bila kujali aina ya kifaa hicho.
Kama wewe nimtumiaji wa simu ya Android ingia Google Play na upakue App hii na uanze furahia kutumia simu yako kama remote kwa vifaa vyako vyote ndani ya nyumba yako.
Pakua hapa : IR Universal Remote
Tecno Camon C9 simu inayotikisa mjini kwa sasa na Camera kali ya Selfie
Kama wewe ni mtumiaji wa simu za Tecno tayari utakuwa unafahamu matoleo
ya Camon ambayo lengo lake kuu ni kumuwezesha mtumiaji wa simu hizo
kupiga picha nzuri na za kuvutia hata kwenye mwanga mdogo.
Tecno Camon C9 ipo tofauti kidogo kwani imekuja na teknolojia ya lens ya F 2.0 ambayo inawezesha mwanga mwingi zaidi kuingia katika kamera na kufanya picha ziwe na mwonekano mzuri zaidi huku ikiwa na Flash mbili ili kuongeza kiasi cha mwanga huo.
Tecno Camon C9 imepakiwa katika kasha zuri la rangi ya bluu na nyeusi ambalo kwa juu lina picha kama ya lens ambayo ni logo ya matoleo ya Camon.

Kwa upande wa kamera ya nyuma C9 inakuja na kamera yenye uwezo sawa na ile ya mbele yaani 13MP huku ikiwa na double flash zilizozungushiwa ndani ya kiduara kuongeza uzuri zaidi.
Simu hii inakuja na Flip Cover kwa ajili ya kulinda kioo chake, pale linapofunikwa kava hili linaweza kukibadilisha kioo cha simu hii kuwa kama saa ya analogia.
Tecno Camon C9 ipo tofauti kidogo kwani imekuja na teknolojia ya lens ya F 2.0 ambayo inawezesha mwanga mwingi zaidi kuingia katika kamera na kufanya picha ziwe na mwonekano mzuri zaidi huku ikiwa na Flash mbili ili kuongeza kiasi cha mwanga huo.
Tecno Camon C9 imepakiwa katika kasha zuri la rangi ya bluu na nyeusi ambalo kwa juu lina picha kama ya lens ambayo ni logo ya matoleo ya Camon.

Nini utavikuta ndani ya Box?
- Simu ya Camon C9
- Chaja ya simu ya ukutani
- USB Cable
- Earpiece kwa ajili ya kusikilizia muziki
- Zana ya kutolea laini (SIM ejector tool)
- Flip Cover
- User manual, Warrant card na Palm chat Flyer
Kamera na Flash
Hapa ndipo sifa ya simu hii inapokuja, ikiwa na kamera ya mbele yenye 13 MP iliyo katikati ya simu itamuwezesha mtumiaji hasa wapenzi wa selfie kupiga picha nzuri na bora zaidi. Uwepo wa kamera katikati ya simu kunaongeza uwezo wa mtumiaji kupiga picha za selfie za makundi kirahisi zaidi. Bila kusahau simu hii ina flash katika kamera ya mbele pia.Kwa upande wa kamera ya nyuma C9 inakuja na kamera yenye uwezo sawa na ile ya mbele yaani 13MP huku ikiwa na double flash zilizozungushiwa ndani ya kiduara kuongeza uzuri zaidi.
Kava na Umbo
Kava la nyuma ni la plastiki ambalo linaweza kufunguliwa ili mtumiaji aweze kuweka laini na Memory kadi yenye uwezo mpaka wa 128GB. C9 imezungukwa na frame ya chuma na kuifanya simu kuwa ya hadhi tofauti na C8, C9 ina vitufe vyote upande mmoja wa simu na kumfanya mtumiaji aweze kuitumia kirahisi zaidi.Simu hii inakuja na Flip Cover kwa ajili ya kulinda kioo chake, pale linapofunikwa kava hili linaweza kukibadilisha kioo cha simu hii kuwa kama saa ya analogia.
Specifications za Simu C9
- HiOS user interface based on Android 6.0 Marshmallow
- Octa Core Processor
- 16GB Rom 2GB Ram
- 5.5″ FHD IPS Touchscreen (1080p)
- 13 MP Front and Back Camera with Flashlight
- Supports LTE Network (4G)
- 3000 mAh Battery
Bei (Shilingi 400,000/=)
Simu hii inapatikana maduka mengi ya jijini Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha kwa sasa kwa bei ya shilingi laki nne za kitanzania (400,000/=).orodha ya simu zitakazofungiwa Whatsapp kuanzia mwaka 2017
orodha ya simu zitakazofungiwa Whatsapp
kuanzia mwaka 2017
Mapema mwaka huu kampuni inayotoa huduma za ujumbe mfupi wa picha, sms, sauti na video ya Whatsapp ilitangaza kufungia huduma kwa baadhi ya simu kutoka katika baadhi ya makampuni kwa madai ya kuboresha zaidi huduma zao.
wa mujibu wa Whatsapp, wameamua kusitisha kutoa huduma kwa baadhi ya simu zinazotumia mifumo endeshi ya kizamani ili kuendana na kasi ya ukuwaji wa soko la simu duniani.
Kwa mujibu wa Whatsapp, simu zitakazositishiwa huduma ni pamoja mwishoni mwa mwaka huu ni pamoja na simu zinazotumia mifumo endeshi ya:-Android : Android 2.1 and Android 2.2
– Windows : Windows Phone 7
– iPhone: 3GS/ iOS 6
Pia whatsapp wamewatahadharisha watumiaji wa simu za,
– Blackberry 10 running on BBOS
– Nokia S40 running on Symbian S40
kuwa kufikia June mwaka 2017 watakuwa wanasitisha kuzipa sapoti simu hizo pia.
Angalia hapa best Android Applications za mwaka 2016 mpaka sasa
Kutafuta application nzuri zaidi katika Play Store ni kazi kidogo.
Haijalishi iwe app ya afya, hali ya hewa au muziki kwa sababu zipo
applications nyingi sana zinazofanya kile unachokihitaji kwa sasa. Leo
katika swahilitech tumejaribu kuangalia zile applications bora zaidi
katika kila nyanja na kujaribu kuzichambua moja moja.

Ukiachana na ES File Explorer kuna Solid File Explorer ambayo kwa sasa inafanya vizuri na inakaribiana kila kitu na ES. Kwa kutumia Solid File Explorer utaweza kuweka vitu katika Dropbox, Drive au OneDrive moja kwa moja. Pia unaweza ukazip, RAR au kuhide mafolder katika simu au tablet yako.

Hapa ndipo Action Launcher 3 inapoingia. Ikiwa na interfae nyepesi na rahisi kutumia action launcher imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya launcher za android.


Best File Manager Application
Bado ES File Explorer inaongoza katika orodha ya applications kali zaidi za kubrowse mafaili. Ikiwa na uwezo wa kuunganisha simu yako na laptop yako kupitia wifi, kucheza miziki na video za kwenye pc yako kupitia kwenye simu yako bila ya kuzisave, uwezo wa kumanage kila kitu katika vifaa vyako bila tabu yoyote ule kunaifanya ES Explorer kuwa App namba moja katika orodha hii.Ukiachana na ES File Explorer kuna Solid File Explorer ambayo kwa sasa inafanya vizuri na inakaribiana kila kitu na ES. Kwa kutumia Solid File Explorer utaweza kuweka vitu katika Dropbox, Drive au OneDrive moja kwa moja. Pia unaweza ukazip, RAR au kuhide mafolder katika simu au tablet yako.

Best Launcher Application
Unapozungumzia muonekano mzuri wa kioo cha simu yako kunaendana moja kwa moja na Launcher unayotumia. Mara nyingi watumiaji wengi wa Android hupendelea kuweka Launcher wanazozifurahia kila wanaposhika simu zao.Hapa ndipo Action Launcher 3 inapoingia. Ikiwa na interfae nyepesi na rahisi kutumia action launcher imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya launcher za android.
Best Application ya Fitness na Mazoezi
Kama wewe ni mpenzi wa mazoezi mazito au mazoezi mepesi mepesi 7 Minute Workout ndio app inayokufaa zaidi. App hii inatilia mkazo katika mazoezi mepesi mepesi yanayojirudia ambayo yamethibishwa kitaalamu kuwa yanasaidia sana katika kupunguza uzito na kukuweka fit masaa yote. Ingia PlayStore uipakue ujionee mwenyewe.Best Android browser app
Hapa ndipo wengi wanapapenda, kukiwa na msururu mrefu wa browsers au vivinjari kama Operamini, UC Browser, Safari, internet Explorer bado Chrome Beta ndio application bora zaidi katika vivinjari. Wepesi wa kuvinjari kunakifanya kivinjari hiki kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani kwa sasa kuliko kivinjari kingine chochote kile.
Angalia Channeli DSTV kwenye simu yako ya Android bure
Nadhani kila mtu anatamani kuwa na DSTV nyumbani kwake ili kufurahia
vipindi vyenye radha tofauti kutoka katika channeli Zaidi ya 245 kutoka
mataifa mbalimbai duniani, tatizo kubwa ni gharama kubwa inayotozwa na
Dstv katika vifurushi vyake. TopServiceCare tumeliona hilo na tumeamua
kukusogezea Dstv kiganjani mwako.

Hakuna asiyejua ubora wa vipindi kutoka katika Channel za Dstv kwa wapenzi wa mpira, wapenzi wa music, wapenzi wa movie pamoja na wapenzi wa habari, maisha na dini. Kwa kutumia njia hii unaweza kuangalia Zaidi ya channel 1000 kutoka duniani kote kwenye simu yako ya android au kwenye Laptop yako.
Ngoja tuende moja kwa moja kwenye pointi, tunaweza kuangalia channeli zote hizi kwa kutumia application inayoitwa Mobdro (Pongezi zote ziende kwa mtengenezaji wa application hii) ambayo haipatikani katika Google Play kwa sababu inakiuka baadhi ya sera za google. Kwa kutumia application hii utaweza kuangalia channeli zote hizo zilizopangwa katika makundi (categories) kama ya Habari, Muziki, Tamthiliya, Movies, Michezo, Magemu, Teknolojia pamoja na nyingine nyingi tu. Kwa kuangalia hayo makundi unaona kila radha tunazopenda kuangalia katika TV zetu zinapatikana.
Nitaorodhesha Channeli 5 katika kila kundi ili uweze kupata picha ya nini utakutana nacho katika application hii,
-Baada ya kumaiza kufanya installation, fungua application yako na taona category tofauti. Hapo utachagua Category na kuanza kuangalia bila tabu yoyote. (Zingatio: Ili kuweza kufurahia application hii ni lazima uwe na kifurushi cha data chenye MB za kutosha na mtandao wenye kasi nzuri kidogo).

Hakuna asiyejua ubora wa vipindi kutoka katika Channel za Dstv kwa wapenzi wa mpira, wapenzi wa music, wapenzi wa movie pamoja na wapenzi wa habari, maisha na dini. Kwa kutumia njia hii unaweza kuangalia Zaidi ya channel 1000 kutoka duniani kote kwenye simu yako ya android au kwenye Laptop yako.
Ngoja tuende moja kwa moja kwenye pointi, tunaweza kuangalia channeli zote hizi kwa kutumia application inayoitwa Mobdro (Pongezi zote ziende kwa mtengenezaji wa application hii) ambayo haipatikani katika Google Play kwa sababu inakiuka baadhi ya sera za google. Kwa kutumia application hii utaweza kuangalia channeli zote hizo zilizopangwa katika makundi (categories) kama ya Habari, Muziki, Tamthiliya, Movies, Michezo, Magemu, Teknolojia pamoja na nyingine nyingi tu. Kwa kuangalia hayo makundi unaona kila radha tunazopenda kuangalia katika TV zetu zinapatikana.
- Habari; Angalia NBS, CNN, FOX NEWS, BLOOMBERG, SKY NEWS pamoja na Al-jazera bure katika simu yako
- Shows; Angalia Adventure time, better call Call, community, regular show, family guy
- Movies; Angalia Movies 24/7, HD Movies, All kinds of movies, Now playing, war movies bure katika simu yako
- Michezo; Angalia ESPN, SKY SPORTS (1,2,3,4,f1), BT SPORTS 1 & 2, Liverpool TV, MUTV, Chelsea TV
- Muziki; Angalia MTV hits UK, The Vault, D17, VEVO hits
Vitu vya kuzingatia kabla ya kuinstall Application hii;
- Simu ya Android yenye toleo la android kuanzia 2.5 na kuendelea.
- Internet
- Application ya Mobdro.
Njia za kufuata ili kuweza kuangalia DSTV Bure katika simu yako
Download (pakua) Application ya Mobdro hapa na install katika simu yako. Kumbuka application hii haipo google pay store hivyo ni lazima uruhusu kuinstall application nje ya play store ili uweze kuinstall application hii. Fanya hivyo kwa kwenda kwenye settings–>Security–>Unknown Sources washa hapo. Kumbuka kuzima hii mara baada ya kuinstall application yako.
-Fungua application yako, kubali user agreement, alafu itakuletea kiwindow kisichokuwa na maandishi, click ok ili kupata version mpya ya application hii.-Baada ya kumaiza kufanya installation, fungua application yako na taona category tofauti. Hapo utachagua Category na kuanza kuangalia bila tabu yoyote. (Zingatio: Ili kuweza kufurahia application hii ni lazima uwe na kifurushi cha data chenye MB za kutosha na mtandao wenye kasi nzuri kidogo).
Mtandao Namba Moja Tanzania unaokuletea habari na mambo mengine yanayohusu teknolojia kwa ujumla kwa lugha ya Kiswahili!
Kiswahili ni Lugha Yetu!
Wasiliana nasi kwa maswali, nafasi ya kutangaza biashara yako au kupata huduma mbali mbali kama kunlock simu yako, Modem yako, Kwa huduma za flyers, Brochures , Computer maintanance , Calendar , Matangazo ya video kwaajiri ya biashara yako
Unlock Simu Yako Leo
Unlock Simu Yako Leo
HUAWEI ASCEND Y600, Y550, Y530 , Y330 , Y300, Y200, Y201,Y101,TiGO
VODAFONE VF 685, V685, SMART KICKA, VodaCom
VODAFONE V875 , V785 VodaCom
TECNO H6 TiGO.
HUAWEI MOBILE Wi-Fi E5331 VodaCom, E5221 TiGO, ZTE R206z VodaCom
1.Je una simu au mobile wi-fi , wireless router , mi-fi yoyote kati ya hizo zilizotajwa hapo juu?
2. Je inatumia SIM CARD ya mtandao mmoja tu?
3. je unataka itumie mitandao yote bila kubagua?
Kama majibu yako ni ndio basi leo umepata suluhisho la matatizo yako
Basi leo umekutana na TOPSERVICECARE ambao ni wataalamu wa ku-unlock simu na vifaa vingine ili viweze kutumia mitandao yote. Tuna-unlock simu zote kwa kutumia unlock codes. Kwa wale wote wenye simu za HUAWEI na zinatumia line moja tu e.g. TiGO, au simu zote za VODAFONE zinazotumia line moja ya VodaCom tu basi wataweza kutumia mitandao yote yaani VodaCom, Airtel, TiGO, Zantel, TTCL, na mitandao yote duniani kote.
.
NITAJUAJE KWAMBA SIMU YANGU INATUMIA MTANDAO MMOJA TU?
Utakapowasha simu yako ikiwa na SIM card tofauti itakutaka kuingiza namba moja wapo kati ya hizi zilizoorodheshwa hapa chini:-
---SIM network unlock pin
--- SIM service provider unlock pin
--- Network unlock code
-- Enter SIM Me Lock Code[NP]
-- Unlock Sim Block
-- Please Input Network Pin
-- SIM locked
--- SIM card locked! Please contact your operator! Reset Key?
QN1.NI TSH NGAPI HUDUMA HII?
Huduma hii ni sawa na bure kabisa. Ni Tsh 8000/= tu. Bei zetu hazina punguzo.
QN2.INAKUWAJE KAMA UNLOCK CODE NITAKAZOPEWA HAZITAFANYA KAZI?
Unlock code zinazotolewa ni "" FACTORY UNLOCK CODE"" , maana yake ni kwamba code hizi ni maalumu kwa simu husika tu na zinategema IMEI ya simu husika. IMEI inapatikana kwenye simu yako kwa kupiga *#06#.Hivyo basi unlock code kutoka TOPSERVICECARE kamwe haziwezi kushindwa kuifungua simu yako . Kila simu inakuwa na unlock code yake tofauti na zingine. Tangu tuanze huduma hii hakuna simu iliyowahi kushindikana hata moja.
QN3.JE KAMA NILIWAHI KUJARIBU KUINGIZA UNLOCK CODE ZA UONGO MPAKA SIMU IKAFUNGWA(BLOCKED) IKAANDIKA "UNLOCK SIM BLOCK" , JE NIFANYEJE?
kwa sasa hatuna huduma kwaambazo zimekuwa blocked.
QN4.JE SIMU ITAJIFUNGA TENA MTANDAO KWA SIKU ZIJAZO BAADA YA KU-UNLOCK AU NIKI-RESET SIMU?
HAPANA. Hata kama ukireset simu au ukiiformat au ukienda nayo nje ya nchi bado itaendelea kutumia mitandao yote duniani kote. Hii ndio maana ya unlocking.
Kwa wale watakaotaka kupata maelekezo ya ziada wanaweza wakawasiliana nasi kwa namba hiii ya simu ya mkononi..
VodaCom: 0757426730
HUAWEI ASCEND Y600, Y550, Y530 , Y330 , Y300, Y200, Y201,Y101,TiGO
VODAFONE VF 685, V685, SMART KICKA, VodaCom
VODAFONE V875 , V785 VodaCom
TECNO H6 TiGO.
HUAWEI MOBILE Wi-Fi E5331 VodaCom, E5221 TiGO, ZTE R206z VodaCom
1.Je una simu au mobile wi-fi , wireless router , mi-fi yoyote kati ya hizo zilizotajwa hapo juu?
2. Je inatumia SIM CARD ya mtandao mmoja tu?
3. je unataka itumie mitandao yote bila kubagua?
Kama majibu yako ni ndio basi leo umepata suluhisho la matatizo yako
Basi leo umekutana na TOPSERVICECARE ambao ni wataalamu wa ku-unlock simu na vifaa vingine ili viweze kutumia mitandao yote. Tuna-unlock simu zote kwa kutumia unlock codes. Kwa wale wote wenye simu za HUAWEI na zinatumia line moja tu e.g. TiGO, au simu zote za VODAFONE zinazotumia line moja ya VodaCom tu basi wataweza kutumia mitandao yote yaani VodaCom, Airtel, TiGO, Zantel, TTCL, na mitandao yote duniani kote.
.
NITAJUAJE KWAMBA SIMU YANGU INATUMIA MTANDAO MMOJA TU?
Utakapowasha simu yako ikiwa na SIM card tofauti itakutaka kuingiza namba moja wapo kati ya hizi zilizoorodheshwa hapa chini:-
---SIM network unlock pin
--- SIM service provider unlock pin
--- Network unlock code
-- Enter SIM Me Lock Code[NP]
-- Unlock Sim Block
-- Please Input Network Pin
-- SIM locked
--- SIM card locked! Please contact your operator! Reset Key?
QN1.NI TSH NGAPI HUDUMA HII?
Huduma hii ni sawa na bure kabisa. Ni Tsh 8000/= tu. Bei zetu hazina punguzo.
QN2.INAKUWAJE KAMA UNLOCK CODE NITAKAZOPEWA HAZITAFANYA KAZI?
Unlock code zinazotolewa ni "" FACTORY UNLOCK CODE"" , maana yake ni kwamba code hizi ni maalumu kwa simu husika tu na zinategema IMEI ya simu husika. IMEI inapatikana kwenye simu yako kwa kupiga *#06#.Hivyo basi unlock code kutoka TOPSERVICECARE kamwe haziwezi kushindwa kuifungua simu yako . Kila simu inakuwa na unlock code yake tofauti na zingine. Tangu tuanze huduma hii hakuna simu iliyowahi kushindikana hata moja.
QN3.JE KAMA NILIWAHI KUJARIBU KUINGIZA UNLOCK CODE ZA UONGO MPAKA SIMU IKAFUNGWA(BLOCKED) IKAANDIKA "UNLOCK SIM BLOCK" , JE NIFANYEJE?
kwa sasa hatuna huduma kwaambazo zimekuwa blocked.
QN4.JE SIMU ITAJIFUNGA TENA MTANDAO KWA SIKU ZIJAZO BAADA YA KU-UNLOCK AU NIKI-RESET SIMU?
HAPANA. Hata kama ukireset simu au ukiiformat au ukienda nayo nje ya nchi bado itaendelea kutumia mitandao yote duniani kote. Hii ndio maana ya unlocking.
Kwa wale watakaotaka kupata maelekezo ya ziada wanaweza wakawasiliana nasi kwa namba hiii ya simu ya mkononi..
VodaCom: 0757426730
Tangaza Nasi
Tangaza Nasi
TopServiceCare Team inatoa huduma kwa wanachi wote.
TopServiceCare Team inategemea Matangazo ilikujiendesha, Tunakaribisha matangazo ya ainazote. wasiliana nasi.
Asante sana kwa mchango wako kwa kutangaza biashara yako kwa kutumia
TopServiceCare.
Monday, November 14, 2016
Tazama Tv online Kwa Simu yako
Unaweza ukaidownload
kwa kubonyeza link hiyo chini, Kuna channel zaidi ya 20, zikiwemo azam
one,azam two,Azam sports HD, Super Sport 1,2,3, na nyingine nyingi,
unapo-install itabidi uruhusu instalation from unknown sources, kwa kuwa
haijawekwa bado play store na pia maboresho yanaendelea
Bonyeza link uidownload
https://www.dropbox.com/s/qwzi7aaci45037l/Online%20Tv.apk?dl=0
Bonyeza link uidownload
https://www.dropbox.com/s/qwzi7aaci45037l/Online%20Tv.apk?dl=0
Wednesday, November 4, 2015
Una Uwezo Mkubwa Na Akili Za Kufanya Kile Unachotaka, Vitumie
Habari mpenzi msomaji wa TOPSERVICECARE. Ni matumaini yangu kuwa mpo salama , ni wakati mwingine tena tunakutana kwa ajili ya kuzidi kujifunza na kukumbushana namna sahihi ya kuangalia mambo. Ndugu yangu napenda nikukumbushe kuwa wewe umeumbwa ukiwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo, ulipewa akili na uwezo wa kufanya kile unatakiwa kufanya hapa duniani.
![]() |
| UNAWEZA. |
Kuna wakati unakutana na mambo ya kusikitisha na kuumiza pale ambapo mtu anakuwa kama amezipeleka akili zake likizo, au naweza sema amejisahau au kujipoteza kabisa , haelewi hata ni nani, anaenda wapi?, kwa nini yupo? n.k. Baadhi ya watu wapo tu kwa kuwa wapo. Baadhi ya watu hawaelewi hata uwezo walio nao, hawajui kusudi la wao kuwepo hapa duniani, mwingine anafikiri alikuja hapa ili aishie kutamani kuwa kama wengine, hajui kama naye ikiwa atatembea na kukaa kwenye ile nafasi yake anacho kitu cha maana , cha
kumfanya na wengine watamani kuwa kama yeye, japo ukweli ni kwamba hakuna mtu awaye yote duniani hapa anaweza kuwa kama wewe ndugu yangu, wewe ni wewe, ni wa peke yako, uliumbwa hivyo kwa kusudi maalumu, Kama ulikua haujui hilo ndio nimekujulisha leo na ikiwa ulisahau basi nakukumbusha tu kuwa hakuna aliye kama wewe, usijifananishe na mwingine wala usitamani kuwa kama yule maana hauwezi kuwa vile, utakuwa unajichosha na kujichelewesha kufika kule unaenda tu, tafuta na tamani kuwa kama wewe yule Muumba alikukusudia uwe, tafuta kujua na kuona ule uwezo umeumbwa nao ndugu yangu, tambua zile akili umepewa ndugu yangu.
Ni jambo la kusikitisha pale unapokutana na mtu anasema kwa kujiamini kabisa kuwa hawezi kufanya jambo fulani na ukitaka kujua ni kwa nini atakuambia eti kwa kuwa fulani alijaribu akashindwa, yaani kwa kuwa tu yule alishindwa naye anaamini atashindwa, anakubali kushindwa bila hata kujaribu kufanya kile kitu, anajipima kwa kumwangalia mtu yule, anajiona yeye hawezi kufanya zaidi ya yule, ndugu yangu tambua kuwa katika maisha haya usitumie kushindwa kwa mwingine kama kipimo cha kwamba nawe huwezi kwenda zaidi ya pale, kwamba hauwezi kufanya zaidi yake, tambua utofauti uliopo miongoni mwetu wanadamu wote, tuna uwezo tofauti wa kufanya mambo, hata namna ya kufikiria tunatofautiana.
Mwingine anashindwa kwa kuwa tu kachagua kushindwa, ninasema kachagua kushindwa kwa maana ya kwamba kama mtu unatumia kigezo cha kwamba kama na yule kashindwa basi na mimi siwezi, mtu huyu ameamua na kuchagua kushindwa lakini angeamua kuangalia kushindwa kwa mwenzie kwa namna tofauti angeweza kufanya vizuri zaidi. Badala ya kukubali kushindwa kwa kuwa yule kashindwa au alishindwa unaweza kuamua kumfuata yule aliyeshindwa na uweze kuchunguza na kuelewa ni kwa nini alishindwa na kuanzia hapo unaweza kupata vitu vya kukufanya wewe hata ukiamua kufanya hilo ufanye kwa uzuri na usahihi zaidi, maana unajua wapi mwenzio aliangukia, unakuwa na nafasi ya kurekebisha.
Lakini pia ukitambua kuwa wanadamu tunaomba mambo yale yale kwa utofauti hautalinganisha uwezo wako na wa yule, utatambua kuwa wewe ni wewe na yule ni yule, lakini ukielewa kuwa muumba wako amekupa uwezo , akili na nguvu za kufanya kile anataka ufanye hautajilinganisha na wengine, hautajipima kwa kuangalia yule kafanya nini. Maana cha muhimu ni wewe kutambua uwezo wako, nafasi yako na kusimama hapo, kufanya kila jambo kuendana na nafasi yako, kujiona wewe kama wewe na kuona kuwa unao uwezo wa kufanya kile umeumbwa uje kufanya, ni vyema kuuliza, kuomba ushauri kwa wengine lakini katika hayo usisahau akili zako, au kuna ule usemi unasema ukiambiwa changanya na zako, pima , jihoji angalia kama ni kweli, kinafaa kwako, usiwe ni mtu wa ndio kila wakati, chunguza mambo, pima, amua.
Ndugu yangu hata ukiambiwa kitu usiwe ni mtu wa kukubali tu, kubali ikiwa kweli kinakubalika na una sababu ya msingi ya kukubali ikiwa kinyume kuwa mkweli na uonyeshe kile unaona na kuamini, usiogope kusema ukweli, usiogope kusimamia kile akili yako inakuridhisha kuwa ni kweli na sahihi hata kama hakuna mtu anayekuelewa lakini ikiwa dhamiri yako haikuhukumu uwe na amani na kusimamia hapo, usifanye jambo kwa kufuata mkumbo, fanya kwa kuwa una uhakika ndicho kitu unahitaji na ni kitu sahihi.
ZIJUE FAIDA NNE ZA KUJENGA NYUMBA KWA KUTUMIA RAMANI YA NYUMBA
Mfano: Wewe ni mwenyeji katika eneo fulani na unamfahamu mzee mmoja katika eneo hilo anaitwa Mzee Mwamba, basi mara ukakutana na mtu mmoja akakauulizia kuhusu mzee huyo na akakuomba umwelekeze mahali anapoishi mzee huyo, bila shaka utaanza kumwelekeza: nyooka na barabara hii kama mita hamsini hivi mbele utaona barabara inakunja kona kuelekea kulia nenda nayo hiyo barabara kama mita miambili hivi utaona jengo kubwa jeupe mkono wa kushoto halafu mkabala na jengo hilo utaona duka la vifaa vya ujenzi, uliza hapo dukani watakuonesha nyumba ya huyo mzee.
Hayo maelekezo uliyoyatoa ni ramani sema tu hujaichora na ukiamua kuichora utaiona kama zilivyo ramani za kawaida.
Kwa mantiki hiyo kila mtu kichwani mwake ana ramani nyingi sana nzuri zenye manufaa kwake na kwa taifa kwa ujumla na laiti ramani hizo zingechorwa tungekuwa na maktaba kubwa ajabu na wakati mwingne hata sehemu ya kuhifadhi zisingetosha.
Maisha ya kila siku.
Unapotaka kuishi kwako yaani katika nyumba yako mwenyewe kuna ramani ya nyumba yako ungependa iwe yaani mwonekano, rangi, ukubwa na hata mwelekeo (orientation) wake. Ungependa umpate mtu mwenye uwezo wa kuionesha ramani hiyo iliyoko kichwani mwako na kisha uipate na uanze hatua ya kuijenga ili uipate ile furaha unayodhani utaipata mara nyumba hiyo itakapo kamilika.
Itakusaidia kukadria gharama za ujenzi.
Maadamu ramani hiyo itakuwa imeonesha vipimo vya “material” ya ujenzi itakuwa rahisi kujua idadi ya bati, matofali, madirisha,nk hii itasaidia kukufanya ujipange vizuri kabla ya kuanza ujenzi.
Ni kiambatisho muhimu katika kupata kibali cha ujenzi.
Kwa mujibu wa sheria ya ujenzi wa majengo inataka ili mtu apate kibali cha ujenzi wa jengo lolote ni lazima aambatanishe katika maombi yake ramani ya jengo analotaka kujenga. Ramani hii itasainiwa na Afisa mipango miji, afisa ardhi na bwana afya na kamati ya ujenzi ya wilaya/mji/manispaa/jiji. nk
Ramani ya nyumba ni kielelezo muhimu katika taasisi za mikopo.
Ukitaka kuchukua mkopo benki au katika taasisi za mikopo na hasa ukitaka kuweka nyumba kama dhamana watahitaji kuiona ramani ya nyumba yako na watahitaji kuiambatanisha katika barua yako ya maombi ya mkopo huo.
Hizo ndizo faida kuu nne za kujenga nyumba kwa kutumia ramani ya nyumba ingawaje zinaweza kuwepo nyingine nyingi, ikumbukwe kuwa kujenga nyumba bila ramani ni sawa na kulima shamba kubwa bila kujua utapanda nini katika shamba hilo, ni hatarii.
TOPSERVICECARE tunaamini kuwa “Kile akili ya binadamu inakiwaza na kukiamini, akili ya binadamu inaweza kukipata”.Na tena, Mtu mmoja mwenye ujasiri ni watu wengi
Tunakuhamasisha ili ufikie mafanikio yako
NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI WA NYUMBA ILI USIJE UKAPIGWA STOP WAKATI WA UJENZI WA NYUMBA YAKO
Kutokana na kuongezeka kwa ujenzi holela sehemu za mijini, Serikali iliamua kuandaa sheria ya mipango miji inaitwa “Sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007”. Sheria hiyo inaelekeza namna ya upangaji wa miji. Moja ya maagizo ya sheria hiyo inamtaka kila mtu anayejenga nyumba kwenye eneo liliotangazwa kuwa eneo la mipango miji awe na kibali cha ujenzi na asipokuwa na kibali hicho hatua zaidi huchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kujenga.
Kwa kufuata maagizo ya sheria hiyo kila halmashauri nchini huandaa sheria ndogo ndogo (by laws) za namna ya utoaji wa kibali hicho cha ujenzi. Sheria hizi ndogo ndogo hutofautiana kutoka halmashauri moja hadi nyingine. Lakini angalau huwa kuna mlolongo unaokaribiana katika utoaji kibali hicho. Nachukua nafasi hii kukushrikisha mlolongo (hatua) za kupata kibali hicho.
Hatua ya kwanza: Andaa Ramani Ya Nyumba Utakayoijenga
Unatakiwa kuwa na ramani ya nyumba utakayo ijenga. Ramani unaweza kuipata kwa mtu yeyote anayechora ramani za nyumba mfano anaweza kuwa Msanifu ramani, au Msanifu Majengo anaweza kukuchorea ramani nzuri.
Hatua Ya Pili: Ramani Hiyo Inatakiwa Kuidhinishwa Na Msanifu Majengo (Architect) Aliyesajiliwa.
Lengo la Msanifu Majengo kuiidhinisha ramani hiyo ni ili kuangalia ubora na vigezo muhimu vinavyotakiwa kwenye nyumba. Pia likitokea tatizo kwenye nyumba hiyo Archtect atawajibika kujibu ikiwa tatizo hilo litatokana na kosa la mchoro wa nyumba hiyo. Wasanifu majengo waliosajiriwa wako wengi kwenye kila mkoa. Ulizia tu utawapata, kinachotakiwa Msanifu majengo huyo atapiga mhuri wake aliopewa na Bodi ya usajiri wa wasanifu majengo kwenye kila ukurasa wa ramani hiyo.
Huwa kuna gharama kidogo kwenye kuidhinisha ramani kwa architect kulingana na aina ya ramani, mfano kama ni ramani ya nyumba ya kuishi yenye vyumba vitatu au vine kuna wengine huwa wanafanya shilingi 50,000/= na wakati mwingine huwa zaidi ya hapo.
Hatua Ya Tatu: Chukua Fomu Kutoka Ofisi Ya Ujenzi Na Uzipitishe Zisainiwe Kila Sehemu Inayohitajika
Fomu hizi zinatakiwa zipitishwe kwa Afisa Ardhi wa Wilaya husika, kwa Afisa Mipango Miji na kwa Bwana Afya wa Wilaya. Sehemu hizo zote kila mmoja atakagua mambo yake. mfano, Afisa Ardhi atakagua kama kiwanja kinamilikiwa kihalali na kinalipiwa kodi ndio maana unatakiwa uambatanishe na Hati au Offer ya kumiliki kiwanja na risiti ya malipo ya kodi ya kiwanja ya hivi karibuni.
Afisa Mipango Miji atakagua aina ya nyumba unayotaka kujenga na matumizi yake na atalinganisha kwenye ramani ya mipango miji ajue eneo unalotaka kujenga hiyo nyumba linepangiwa matumizi gani. Kama eneo unalotaka kujenga limetengwa kwa ajili ya viwanda na wewe unataka kujenga nyumba ya makazi hata kubali kusaini kwenye sehemu yake. Bwana Afya atakagua ukubwa wa madirisha na uhusiano wa matumizi ya chumba kimoja na kingine. Pia atakagua shimo la maji taka (septic tank). Ukimaliza kupitisha huko utairudisha fomu hiyo ofisi ya ujenzi.
Hatua Ya Nne: Kutembelea Kiwanja Na Kujiridhisha.
Baada ya hapo Mhandisi wa Ujenzi itabidi uende naye kwenye kiwanja unachotaka kujenga ili akajaze taarifa za kiwanja chako na akajiridhishe kama kiwanja kweli kipo. Taarifa ya kiwanja chako atazijaza kwenye fomu hizo kuna sehemu ya kujaza Mhandisi wa Ujenzi. Halafu atapiga mhuri wa ofisi ya ujenzi kama ishara ya kwamba kila kitu kiko vizuri.
Hatua Ya Tano: Kuidhinishwa Na Kamati Ya Ujenzi Ya Wilaya Husika.
Mhandisi wa ujenzi akisha kagua kiwanja chako na akajaza taarifa zake kwenye fomu, kinachofuata ramani hiyo na fomu zote itapelekwa kwenye kikao cha kamati ya ujenzi ya Wilaya ambacho hukaa mara moja kila baada ya muda fulani mfano kuna baadhi ya halmashauri kamati hiyo hufanya kikao chake kila baada ya miezi mitatu. Kikao hicho ndicho kitaidhinisha kutolewa kwa kibali cha ujenzi wa nyumba unayotaka kujenga.
Hatua Ya Sita: Kibali Kinatolewa.
Mara baada ya kikao cha kamati ya ujenzi kumalizika, vibali vyote vilivyoidhinishwa kutolewa, hutolewa kwa wahusika. Kinachotakiwa wakati wa mchakato wote huo uwe na nakala 3 au 4 za ramani yako ya nyumba ili mara baada ya kutolewa kwa kibali cha ujenzi nakala moja atabaki nayo mwenye nyumba, nakala nyingine itapelekwa Ofisi ya Ardhi ya wilaya na nakala moja itabaki kwenye Ofisi ya Ujenzi kama kumbukumbu.
Ukipata kibali chako unaweza kuendelea na ujenzi wako kwa amani bila bughuza. Kutokuwa na kibali cha ujenzi ukibainika unaweza kuzuiliwa kujenga (stop order) mpaka utakapopata kibali cha ujenzi.
“Moja ya maagizo ya sheria hiyo inamtaka kila mtu anayejenga nyumba kwenye eneo liliotangazwa kuwa eneo la mipango miji awe na kibali cha ujenzi na asipokuwa na kibali hicho hatua zaidi huchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kujenga”
Tunakutakia kila la heri katika ujenzi wa Taifa. TOPSERVICECARE
Saturday, October 31, 2015
Hizi ndizo faida 50 za mazoezi
Moja ya mahitaji matano (5) mhimu ili kuishi baada ya oksijeni, maji, chumvi, na potasiamu; ni Mazoezi. Mazoezi ni mhimu kwa ajili ya afya zaidi ya kuwa na maumbile ya kuvutia (sex body), burudani au kitu kingine chochote.
Watu wengi hufuatilia kuhusu chakula tu, hata kama utakula vizuri vipi bila mazoezi mlo haujakamilika, kwa hiyo mazoezi ni mhimu kwa yeyote kama ilivyo kwa maji au chakula.
Hizi ndizo faida 50 za mazoezi
Zifuatazo ni moja ya sababu 50 mhimu za kufanya mazoezi kwa afya bora na maisha marefu bila maumivu:
1. Hukufanya ujisikie vizuri
2. Huongeza uwezo wa kujifunza
3. Hujenga uwezo wa kujistahi
4. Huongeza nguvu ya ubongo kufanya kazi
5. Huuweka mwili wako kuwa unaofaa (fit) na wenye uwezo
6. Huongeza afya ya akili yako
7. Huongeza kinga ya mwili
8. Hupunguza mfadhaiko/stress
9. Hukufanya ujisikie vizuri/mwenye furaha
10. Hukufanya usizeeke mapema
11. Huweka ngozi yenye mng’aro na yenye afya
12. Husaidia kupata usingizi mtulivu
13. Husaidia kuzuia ugonjwa wa kiharusi/strokes
14. Huongeza ufanisi katika makutano/joints ya mwili
15. Huongeza nguvu za mishipa
16. Huondoa wasiwasi
17. Huongeza kumbukumbu
18. Husaidia kudhibiti ulevi/uteja
19. Huongeza uzarishaji
20. Huongeza uwezo wa ubunifu
21. Hupendezesha muonekano wa mwili
22. Huongeza uwezo wa kujiamini
23. Husaidia kuongeza nguvu juu ya malengo yako maishani
24. Huondoa tatizo la kukinaishwa na chakula
25. Huongeza miaka ya kuishi
26. Hukomaza mifupa
27. Huongeza afya ya moyo
28. Huongeza hali ya kuwa na msimamo
29. Huondoa homa ndogo ndogo mwilini
30. Huongeza hamu ya kula
31. Hudhibiti usawa wa lehemu/kolesteroli
32. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi ya kansa
33. Hushusha shinikizo la juu la damu/BP
34. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
35. Huzuia kupatwa na ukichaa/uwendawazimu
36. Hupunguza au huzuia maumivu ya mgongo
37. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa mifupa
38. Hupunguza hisia/fikra za kujisikia vibaya au huzuni
39. Huzuia kupotea kwa mishipa
40. Huongeza nguvu na ustahimilivu
41. Huongeza ufanisi katika michezo
42. Huongeza uwezo wa kuvumilia maumivu
43. Huongeza usawa na ushirikiano wa mwili
44. Huongeza usambazaji wa oksijeni katika seli za mwili
45. Huongeza hali ya ufuatiliaji/concentration
46. Huongeza uwezo wa kujitawala na kujidhibiti nafsi
47. Huondoa uchovu
48. Huongeza nguvu katika tendo la ndoa
49. Hufanya maisha ni yenye kuvutia zaidi
50. Huongeza ubora wa maisha
2. Huongeza uwezo wa kujifunza
3. Hujenga uwezo wa kujistahi
4. Huongeza nguvu ya ubongo kufanya kazi
5. Huuweka mwili wako kuwa unaofaa (fit) na wenye uwezo
6. Huongeza afya ya akili yako
7. Huongeza kinga ya mwili
8. Hupunguza mfadhaiko/stress
9. Hukufanya ujisikie vizuri/mwenye furaha
10. Hukufanya usizeeke mapema
11. Huweka ngozi yenye mng’aro na yenye afya
12. Husaidia kupata usingizi mtulivu
13. Husaidia kuzuia ugonjwa wa kiharusi/strokes
14. Huongeza ufanisi katika makutano/joints ya mwili
15. Huongeza nguvu za mishipa
16. Huondoa wasiwasi
17. Huongeza kumbukumbu
18. Husaidia kudhibiti ulevi/uteja
19. Huongeza uzarishaji
20. Huongeza uwezo wa ubunifu
21. Hupendezesha muonekano wa mwili
22. Huongeza uwezo wa kujiamini
23. Husaidia kuongeza nguvu juu ya malengo yako maishani
24. Huondoa tatizo la kukinaishwa na chakula
25. Huongeza miaka ya kuishi
26. Hukomaza mifupa
27. Huongeza afya ya moyo
28. Huongeza hali ya kuwa na msimamo
29. Huondoa homa ndogo ndogo mwilini
30. Huongeza hamu ya kula
31. Hudhibiti usawa wa lehemu/kolesteroli
32. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi ya kansa
33. Hushusha shinikizo la juu la damu/BP
34. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
35. Huzuia kupatwa na ukichaa/uwendawazimu
36. Hupunguza au huzuia maumivu ya mgongo
37. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa mifupa
38. Hupunguza hisia/fikra za kujisikia vibaya au huzuni
39. Huzuia kupotea kwa mishipa
40. Huongeza nguvu na ustahimilivu
41. Huongeza ufanisi katika michezo
42. Huongeza uwezo wa kuvumilia maumivu
43. Huongeza usawa na ushirikiano wa mwili
44. Huongeza usambazaji wa oksijeni katika seli za mwili
45. Huongeza hali ya ufuatiliaji/concentration
46. Huongeza uwezo wa kujitawala na kujidhibiti nafsi
47. Huondoa uchovu
48. Huongeza nguvu katika tendo la ndoa
49. Hufanya maisha ni yenye kuvutia zaidi
50. Huongeza ubora wa maisha
Mazoezi yafuatayo ni mazuri sababu ya thamani yake ya baadaye na hayasababishi maumivu kwenye maungio, nayo ni; kutembea kwa miguu, kuogelea, kuendesha baiskeli, kucheza tenisi, gofu, kukwea, kudansi na kadharika.
Kitunguu Swaumu hutibu magonjwa 30
MUNGU anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na ustawi wetu. Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.
Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika majikikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
Kigawanyishe katika punje punje
Menya nusu yake (punje 8 au 10 hivi),
Menya punje moja baada ya nyingine
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu
Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2 kama unaumwa na moja wapo ya magonjwa niliyoyaorodhesha hapa chini.
Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30
Haya ni baadhi ya magonjwa yanayotibika au kukingika na kitunguu swaumu:
- Huondoa sumu mwilini
- Husafisha tumbo
- Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
- Husafisha njia ya mkojo
- Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria
- Huzuia kuhara damu (Dysentery)
- Huondoa Gesi tumboni
- Hutibu msokoto wa tumbo
- Hutibu Typhoid
- Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
- Hutibu mafua na malaria
- Hutibu kifua kikuu
- Hutibu kipindupindu
- Hutibu upele
- Huvunjavunja mawe katika figo
- Hutibu mba kichwani
- Huupa nguvu ubongo
- Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
- Huongeza SANA nguvu za kiume
- Hutibu maumivu ya kichwa
- Hutibu kizunguzungu
- Hutibu shinikizo la juu la damu
- Huzuia saratani/kansa
- Hutibu maumivu ya jongo/gout
- Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
- Huongeza hamu ya kula
- Huzuia damu kuganda
- Husaidia kutibu kisukari
- Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi
- Huongeza SANA kinga ya mwili
UFAHAMU WAKATI MZURI WA KUPATA MAWAZO MAPYA NA KUJIONA MWENYEWE
Habari Ndugu:
Katika maisha yako umesha chunguza na ukafahamu ni wakati gani huwa unapata mawazo mapya au ni wakati gani huwa unajisikia furaha utulivu wa akili na hatimaye unapata nguvu mpya ya kusonga mbele kwenye maisha yako? Je, ni wakati ukiwa umelala?, ni wakati ukiwa unaangalia mpira?, ni wakati ukiwa na rafiki yako? Ni wakati ukiwa baa? Au ni wakati gani?
Dunia imejaa kelele nyingi kila mahali, kuna kelele za magari, kuna kelele za watu, kuna kelele za mihemko ya mwili na kuna kelele za wanyama na ndege
wa angani. Tunayo bahati kubwa sana miili yetu inauwezo wa kuchuja hizo kelele na hatimaye hazikuathiri sana lakini katikati ya kelele hizo ni vigumu sana kupata wazo jipya na kujiona mwenyewe. Pia katikati ya kelele hizo ni vigumu sana kupata nguvu mpya.
Kuna rafiki yangu mmoja nilimwuliza hivi; “Ni wakati gani huwa unapata mawazo mapya?” “Akasema kwa kweli mara nyingi sana nikiwa naangalia mpira huwa napata mawazo mapya na siku nyingine nikiwa napiga stori na marafiki zangu huwa napata mawazo mapya”.
Nikamwuliza kwa namna hii “Ni wakati gani huwa unajiona mwenyewe? Akashangaa! kujiona mwenyewe? Mbona kila siku huwa najiona hata sasa najiona au unamaanisha nini? Nikamwambia sina maana nyingine ni hiyo hiyo ni wakati gani huwa unajiona mwenyewe? Akasema hapo sijakuelewa naomba ufafanuzi.
Nikaanza kumweleza; mara nyingi sana sisi binadamu huwa hatujioni sisi mwenyewe lakini huwa tunawaona watu wengine, pale wanapofanya mambo mazuri wakati mwingine huwa wa kwanza kutoa maoni yetu juu ya mafanikio hayo au wanapofanya vibaya huwa vile vile wa kwanza kutoa maoni yetu juu ya kufanya vibaya kwao. Wakati tunatoa maoni yetu juu ya watu wengine macho yetu na akili zetu huwa zinasahau kujiona (kujiangalia) sisi wenyewe. Kwahiyo kujiona wewe mwenyewe (finding yourself) ni kule kujitambua kutoka ndani
yako sehemu ulipo katika mambo yote, mfano kiuchumi, kiroho, kielimu n.k
Mtu anayejiona yeye mwenyewe anakuwa makini na anakuwa na kiu ya kutaka afike sehemu fulani, hapotezi muda bure kwenye mambo yasiyomsaidia kwenye maisha yake, tena mtu anayejiona yeye mwenyewe sio mwepesi wa kutoa maoni juu ya watu wengine maana kabla hajatoa maoni juu ya watu wengine jicho lake litamwona yeye kwanza. Baada ya maelezo hayo akasema hapo nimekuelewa.
Ninachotaka nikushirikishe ndugu kwenye makala hii ni kwamba kuna wakati ambapo mtu anaweza kujiona yeye mwenyewe wakati huu anapojiona yeye mwenyewe ndipo anapata mawazo mapya yenye kumjenga. Je, ni wakati gani huo?
Ni wakati wa KUPUNGA. Kupunga ndio nini? Kupunga ni wakati ambapo mtu anaenda sehemu tulivu yenye mandhari nzuri na mara nyingi wakati wa jioni au mchana kwa lengo la kutafakari. Mtu huenda kwenye eneo hilo akiwa peke yake. Kupunga ni namna ya kupata mawazo mapya na kujiona wewe mwenyewe na njia hii ilitumiwa tangu enzi za mababu wa kale na kale. Walikuwa wanatumia njia hii ya kupunga kondeni hasa mara baada ya kazi ngumu. Baadaye katika kizazi chetu watu wameanzisha utaratibu wa kwenda
kupunga na marafiki zao sehemu za fukwe ya bahari au ziwa.
Lakini kupunga yenye lengo la kupata mawazo mapya na kujiona wewe mwenyewe unatakiwa uwe peke yako ukitafakari jinsi ulivyo, maisha yako yalivyo, mwelekeo wako utakuwaje lakini pia ukifurahia mandhari nzuri ya uso wa dunia na wakati mwingine miziki ya sauti za ndege ikiimba kwa mbali. Wafalme wengi walitumia njia hii ya kupunga ili kupata utulivu wa akili na utulivu wa moyo katika kutawala kwao na jinsi ya kukabiliana na maadui zao.
Je, wewe huwa unapunga?. Kuna faida nyingi sana za kupunga, mimi baada ya kuzifahamu faida hizo mara nyingi huwa napunga. Utanikuta niko sehemu tulivu yenye mandhari nzuri au wakati mwingine huwa naenda mlimani napanda juu ya mlima halafu naanza kufurahia jinsi dunia ilivyo nzuri, jinsi mimi mwenyewe nilivyo mzuri, si hayo tu bali huwa napata msimamo wa maisha yangu. Toka nikiwa kidato cha kwanza nilianza tabia hii ya kupunga mpaka sasa naendelea, kwa kweli ni furaha kubwa. Naomba nikushirikishe baadhi ya faida unazozipata kwa kupunga.
Kubadili msimamo hasi wa kimawazo.
Kupitia kupunga huwa nabadilika kabisa jinsi ya kufikiri kwangu, wakati mwingine huwa moyoni nimejaa fikira potofu za mahangaiko ya hapa na pale lakini nikienda kupunga nguvu mpya hunijia na mawazo mapya ya kukabiliana na changamoto za maisha yaninijia.
Kupata furaha na raha ya kuishi duniani.
Ni kweli kabisa kama nilivyokudokeza hapo mwanzo, wafalme wengi na mpaka hivi sasa utakuta wana bustani kubwa na nzuri mara nyingi saa za jioni huenda
kwenye bustani zao na kufurahia maisha. Mara nyingi mimi nikiwa napunga huwa nafurahi sana kuona mimi ni mzima mwenye afya na huwa nafurahi sana kuona dunia jinsi ilivyo nzuri. Zaidi ya yote huwa nafurahi sana ninapowasikia na kuowaona ndege jinsi wanavyoimba na kufurahi. Nikiwa napungia ufukweni huwa nafurahi sana kuona jinsi bahari au ziwa linavyopendeza na wakati mwingine nikiwaona viumbe vya bahari wanavyofurahia maisha wakiruka ruka kwenye ulimwengu wao.
Kutoa wivu, hasira na kujaa upendo.
Wakati mwingine huwa tunakwazwa na mambo mengi sana katika maisha. Ukiwa na tabia ya kupunga utashangaa hizo sumu zinatoweka na badala ya kuwa na hizo sumu unakuwa na upendo mwingi. Kwanza unajipenda wewe mwenyewe na unajiona ni mwenye bahati. Lakini pia kama utakuwa unapungia eneo lenye ndege au wanyama, viumbe hao watakufundisha jinsi wanavyoishi kwa kupendana wakifurahi siku zote.
Kujiona wewe mwenyewe.
Hili ndilo lengo hasa la makala hii, wakati wa kupunga ni wakati wa kujiona wewe mwenyewe. Ndio maana nakushauri unapopunga kwa lengo la kujiona wewe mwenyewe unatakiwa uwe peke yako. Wakati ukiwa unatafakari tafakari utashangaa utakapojiona wewe mwenyewe jinsi ulivyo mzuri, ulivyo barikiwa, tena utajiona wewe mwenyewe jinsi unavyotakiwa kuongeza juhudi kwenye mambo yako mazuri nk. Unapokuwa kwenye kelele nyingi sio rahisi kujiona wewe mwenyewe wala hutajigundua jinsi ulivyo. Nakushauri kama unanafasi anza tabia hii ya kupunga utashangaa jinsi utakavyojiona wewe mwenyewe.
Unapokuwa unapunga ufanye nini zaidi?
Unapopunga unatakiwa kuwa kwenye eneo lenye utulivu, ni vizuri ukazima simu yako ili ubaki peke yako. Unapopunga jifurahie wewe mwenyewe, pumua kwa nguvu halafu jisikilizie jinsi ilivyo raha kupumua, utashangaa wakati unapumua kwa namna hii utaona kila kitu kinachokuzunguka jinsi kilivyo kizuri, anga litakuwa zuri miali ya mwanga itakuwa inadunda dunda hata hakuna lugha ya kuielezea.
Ushauri wangu.
Mpendwa msomaji wa Top Service Care nakushauri anza kuwa na tabia ya kupunga angalau tenga hata siku moja kwa wiki saa ya jioni mara baada ya kazi nenda kwenye eneo zuri ukapunge. Kunafaida kubwa sana ya kupunga hata Mungu mwenyewe huwa anapunga saa ya jioni kama ilivyoandikwa kwenye
kitabu cha Mwanzo. Mimi naamini nguvu iliyomo wakati wa kupunga, na nitaendelea siku zote kupunga nipatapo nafasi. Kama hujaanza wala hujawahi kujaribu basi mara umalizapo kusoma makala hii jiwekee ratiba ya kupunga halafu utaniambia jinsi ilivyo raha kupunga. Unaweza kuniandikia kwa email
“Kupunga ni namna ya kupata mawazo mapya na kujiona wewe mwenyewe na njia hii ilitumiwa tangu enzi za mababu wa kale na kale. Walikuwa wanatumia njia hii ya kupunga kondeni hasa mara baada ya kazi ngumu”
Tunakuhamasisha ili ufikie mafanikio yako





















