Monday, December 5, 2016

Angalia hapa best Android Applications za mwaka 2016 mpaka sasa

Kutafuta application nzuri zaidi katika Play Store ni kazi kidogo. Haijalishi iwe app ya afya, hali ya hewa au muziki kwa sababu zipo applications nyingi sana zinazofanya kile unachokihitaji kwa sasa. Leo katika swahilitech tumejaribu kuangalia zile applications bora zaidi katika kila nyanja na kujaribu kuzichambua moja moja.
best android apps













Best File Manager Application

Bado ES File Explorer inaongoza katika orodha ya applications kali zaidi za kubrowse mafaili. Ikiwa na uwezo wa kuunganisha simu yako na laptop yako kupitia wifi, kucheza miziki na video za kwenye pc yako kupitia kwenye simu yako bila ya kuzisave, uwezo wa kumanage kila kitu katika vifaa vyako bila tabu yoyote ule kunaifanya ES Explorer kuwa App namba moja katika orodha hii.
Ukiachana na ES File Explorer kuna Solid File Explorer ambayo kwa sasa inafanya vizuri na inakaribiana kila kitu na ES. Kwa kutumia Solid File Explorer utaweza kuweka vitu katika Dropbox, Drive au OneDrive moja kwa moja. Pia unaweza ukazip, RAR au kuhide mafolder katika simu au tablet yako.
Solid-Explorer-File-Manager


Best Launcher Application

Unapozungumzia muonekano mzuri wa kioo cha simu yako kunaendana moja kwa moja na Launcher unayotumia. Mara nyingi watumiaji wengi wa Android hupendelea kuweka Launcher wanazozifurahia kila wanaposhika simu zao.
Hapa ndipo Action Launcher 3 inapoingia. Ikiwa na interfae nyepesi na rahisi kutumia action launcher imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya launcher za android.


Action-Launcher-3 

Best Application ya Fitness na Mazoezi

Kama wewe ni mpenzi wa mazoezi mazito au mazoezi mepesi mepesi 7 Minute Workout ndio app inayokufaa zaidi. App hii inatilia mkazo katika mazoezi mepesi mepesi yanayojirudia ambayo yamethibishwa kitaalamu kuwa yanasaidia sana katika kupunguza uzito na kukuweka fit masaa yote. Ingia PlayStore uipakue ujionee mwenyewe.


Best Android browser app

Hapa ndipo wengi wanapapenda, kukiwa na msururu mrefu wa browsers au vivinjari kama Operamini, UC Browser, Safari, internet Explorer bado Chrome Beta ndio application bora zaidi katika vivinjari. Wepesi wa kuvinjari kunakifanya kivinjari hiki kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani kwa sasa kuliko kivinjari kingine chochote kile.







browsers










Share:

0 comments:

Post a Comment

Top Servicare. Powered by Blogger.

Web Design

Popular Posts

INSTAGRAM FEED

@soratemplates

Blog Archive

About