Monday, December 5, 2016

Je unajua simu yako ya Android inaweza fanya kazi kama remote control kwenye kifaa chochote kile bila kujali aina ya kifaa (TV,AC, Satellite na DVR).

Je umepoteza remote ya TV,AC, Satellite na DVR ? tumia (IR Blaster Sensor) kwenye simu yako ya Android nautaweza kutumia kama remote bila kuwa na haja ya kuangaika madukani wala kujali Brand ya kifaa. Fata hatua hizi.


remote_SwahiliTech

Kuna aina nyingi sana za TV, AC, Satellite na DVR katika matumizi yetu ya kilasiku. 

Maranyingi imekuwa kazi ngumu sana kupata remote control ya kifaa chako pale inapo potea au kuharibika pia ningumu sana kukuta remote moja unaweza kuitumia kwenye vifaa vyako vyote nyumbani bila kujali aina ya kifaa hicho.

Kama wewe nimtumiaji wa simu ya Android ingia Google Play na upakue App hii na uanze furahia kutumia simu yako kama remote kwa vifaa vyako vyote ndani ya nyumba yako.

 Pakua hapa : IR Universal Remote
Share:

Tecno Camon C9 simu inayotikisa mjini kwa sasa na Camera kali ya Selfie

Kama wewe ni mtumiaji wa simu za Tecno tayari utakuwa unafahamu matoleo ya Camon ambayo lengo lake kuu ni kumuwezesha mtumiaji wa simu hizo kupiga picha nzuri na za kuvutia hata kwenye mwanga mdogo.

Tecno Camon C9 ipo tofauti kidogo kwani imekuja na teknolojia ya lens ya F 2.0 ambayo inawezesha mwanga mwingi zaidi kuingia katika kamera na kufanya picha ziwe na mwonekano mzuri zaidi huku ikiwa na Flash mbili ili kuongeza kiasi cha mwanga huo.

Tecno Camon C9 imepakiwa katika kasha zuri la rangi ya bluu na nyeusi ambalo kwa juu lina picha kama ya lens ambayo ni logo ya matoleo ya Camon.


c9-01


Nini utavikuta ndani ya Box?

  1. Simu ya Camon C9
  2. Chaja ya simu ya ukutani
  3. USB Cable
  4. Earpiece kwa ajili ya kusikilizia muziki
  5. Zana ya kutolea laini (SIM ejector tool)
  6. Flip Cover
  7. User manual, Warrant card na Palm chat Flyer
Simu hii inaumbo zuri linaloshikika kirahisi kiganjani na kwa upande wa nyuma ina umbo kama la yai.

Kamera na Flash

Hapa ndipo sifa ya simu hii inapokuja, ikiwa na kamera ya mbele yenye 13 MP iliyo katikati ya simu itamuwezesha mtumiaji hasa wapenzi wa selfie kupiga picha nzuri na bora zaidi. Uwepo wa kamera katikati ya simu kunaongeza uwezo wa mtumiaji kupiga picha za selfie za makundi kirahisi zaidi. Bila kusahau simu hii ina flash katika kamera ya mbele pia.

Kwa upande wa kamera ya nyuma C9 inakuja na kamera yenye uwezo sawa na ile ya mbele yaani 13MP huku ikiwa na double flash zilizozungushiwa ndani ya kiduara kuongeza uzuri zaidi.

Kava na Umbo

Kava la nyuma ni la plastiki ambalo linaweza kufunguliwa ili mtumiaji aweze kuweka laini na Memory kadi yenye uwezo mpaka wa 128GB. C9 imezungukwa na frame ya chuma na kuifanya simu kuwa ya hadhi tofauti na C8, C9 ina vitufe vyote upande mmoja wa simu na kumfanya mtumiaji aweze kuitumia kirahisi zaidi.

Simu hii inakuja na Flip Cover kwa ajili ya kulinda kioo chake, pale linapofunikwa kava hili linaweza kukibadilisha kioo cha simu hii kuwa kama saa ya analogia.

c9-05

Specifications za Simu C9

  • HiOS user interface based on Android 6.0 Marshmallow
  • Octa Core Processor
  • 16GB Rom 2GB Ram
  • 5.5″ FHD IPS Touchscreen (1080p)
  • 13 MP Front and Back Camera with Flashlight
  • Supports LTE Network (4G)
  • 3000 mAh Battery
c9-07

Bei (Shilingi 400,000/=)

Simu hii inapatikana maduka mengi ya jijini Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha kwa sasa kwa bei ya shilingi laki nne za kitanzania (400,000/=).


Share:

orodha ya simu zitakazofungiwa Whatsapp kuanzia mwaka 2017

orodha ya simu zitakazofungiwa Whatsapp      

                 kuanzia mwaka 2017

 Mapema mwaka huu kampuni inayotoa huduma za ujumbe mfupi wa picha, sms, sauti na video ya Whatsapp ilitangaza kufungia huduma kwa baadhi ya simu kutoka katika baadhi ya makampuni kwa madai ya kuboresha zaidi huduma zao.

whatsapp-messenger 

wa mujibu wa Whatsapp, wameamua kusitisha kutoa huduma kwa baadhi ya simu zinazotumia mifumo endeshi ya kizamani ili kuendana na kasi ya ukuwaji wa soko la simu duniani.

Kwa mujibu wa Whatsapp, simu zitakazositishiwa huduma ni pamoja mwishoni mwa mwaka huu ni pamoja na simu zinazotumia mifumo endeshi ya:

-Android : Android 2.1 and Android 2.2
– Windows : Windows Phone 7
– iPhone: 3GS/ iOS 6

Pia whatsapp wamewatahadharisha watumiaji wa simu za,

– Blackberry 10 running on BBOS
– Nokia S40 running on Symbian S40

kuwa kufikia June mwaka 2017 watakuwa wanasitisha kuzipa sapoti simu hizo pia.

 

Share:

Angalia hapa best Android Applications za mwaka 2016 mpaka sasa

Kutafuta application nzuri zaidi katika Play Store ni kazi kidogo. Haijalishi iwe app ya afya, hali ya hewa au muziki kwa sababu zipo applications nyingi sana zinazofanya kile unachokihitaji kwa sasa. Leo katika swahilitech tumejaribu kuangalia zile applications bora zaidi katika kila nyanja na kujaribu kuzichambua moja moja.
best android apps













Best File Manager Application

Bado ES File Explorer inaongoza katika orodha ya applications kali zaidi za kubrowse mafaili. Ikiwa na uwezo wa kuunganisha simu yako na laptop yako kupitia wifi, kucheza miziki na video za kwenye pc yako kupitia kwenye simu yako bila ya kuzisave, uwezo wa kumanage kila kitu katika vifaa vyako bila tabu yoyote ule kunaifanya ES Explorer kuwa App namba moja katika orodha hii.
Ukiachana na ES File Explorer kuna Solid File Explorer ambayo kwa sasa inafanya vizuri na inakaribiana kila kitu na ES. Kwa kutumia Solid File Explorer utaweza kuweka vitu katika Dropbox, Drive au OneDrive moja kwa moja. Pia unaweza ukazip, RAR au kuhide mafolder katika simu au tablet yako.
Solid-Explorer-File-Manager


Best Launcher Application

Unapozungumzia muonekano mzuri wa kioo cha simu yako kunaendana moja kwa moja na Launcher unayotumia. Mara nyingi watumiaji wengi wa Android hupendelea kuweka Launcher wanazozifurahia kila wanaposhika simu zao.
Hapa ndipo Action Launcher 3 inapoingia. Ikiwa na interfae nyepesi na rahisi kutumia action launcher imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya launcher za android.


Action-Launcher-3 

Best Application ya Fitness na Mazoezi

Kama wewe ni mpenzi wa mazoezi mazito au mazoezi mepesi mepesi 7 Minute Workout ndio app inayokufaa zaidi. App hii inatilia mkazo katika mazoezi mepesi mepesi yanayojirudia ambayo yamethibishwa kitaalamu kuwa yanasaidia sana katika kupunguza uzito na kukuweka fit masaa yote. Ingia PlayStore uipakue ujionee mwenyewe.


Best Android browser app

Hapa ndipo wengi wanapapenda, kukiwa na msururu mrefu wa browsers au vivinjari kama Operamini, UC Browser, Safari, internet Explorer bado Chrome Beta ndio application bora zaidi katika vivinjari. Wepesi wa kuvinjari kunakifanya kivinjari hiki kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani kwa sasa kuliko kivinjari kingine chochote kile.







browsers










Share:

Angalia Channeli DSTV kwenye simu yako ya Android bure

Nadhani kila mtu anatamani kuwa na DSTV nyumbani kwake ili kufurahia vipindi vyenye radha tofauti kutoka katika channeli Zaidi ya 245 kutoka mataifa mbalimbai duniani, tatizo kubwa ni gharama kubwa inayotozwa na Dstv katika vifurushi vyake. TopServiceCare tumeliona hilo na tumeamua kukusogezea Dstv kiganjani mwako.




dstv-mobile-android


Hakuna asiyejua ubora wa vipindi kutoka katika Channel za Dstv kwa wapenzi wa mpira, wapenzi wa music, wapenzi wa movie pamoja na wapenzi wa habari, maisha na dini.  Kwa kutumia njia hii unaweza kuangalia Zaidi ya channel 1000 kutoka duniani kote kwenye simu yako ya android au kwenye Laptop yako.
Ngoja tuende moja kwa moja kwenye pointi, tunaweza kuangalia channeli zote hizi kwa kutumia application inayoitwa Mobdro (Pongezi zote ziende kwa mtengenezaji wa application hii) ambayo haipatikani katika Google Play kwa sababu inakiuka baadhi ya sera za google.  Kwa kutumia application hii utaweza kuangalia channeli zote hizo zilizopangwa katika makundi (categories) kama ya Habari, Muziki, Tamthiliya, Movies, Michezo, Magemu, Teknolojia pamoja na nyingine nyingi tu. Kwa kuangalia hayo makundi unaona kila radha tunazopenda kuangalia katika TV zetu zinapatikana.


Nitaorodhesha Channeli 5 katika kila kundi ili uweze kupata picha ya nini utakutana nacho katika application hii,
  • Habari; Angalia NBS, CNN, FOX NEWS, BLOOMBERG, SKY NEWS pamoja na Al-jazera bure katika simu yako
  • Shows; Angalia Adventure time, better call Call, community, regular show, family guy
  • Movies; Angalia Movies 24/7, HD Movies, All kinds of movies, Now playing, war movies bure katika simu yako
  • Michezo; Angalia ESPN, SKY SPORTS (1,2,3,4,f1), BT SPORTS 1 & 2, Liverpool TV, MUTV, Chelsea TV
  • Muziki; Angalia MTV hits UK, The Vault, D17, VEVO hits

Vitu vya kuzingatia kabla ya kuinstall Application hii;

  1. Simu ya Android yenye toleo la android kuanzia 2.5 na kuendelea.
  2. Internet
  3. Application ya Mobdro.

Njia za kufuata ili kuweza kuangalia DSTV Bure katika simu yako

 Download (pakua) Application ya Mobdro hapa na install katika simu yako. Kumbuka application hii haipo google pay store hivyo ni lazima uruhusu kuinstall application nje ya play store ili uweze kuinstall application hii. Fanya hivyo kwa kwenda kwenye settings–>Security–>Unknown Sources washa hapo. Kumbuka kuzima hii mara baada ya kuinstall application yako.

-Fungua application yako, kubali user agreement, alafu itakuletea kiwindow kisichokuwa na maandishi, click ok ili kupata version mpya ya application hii.

-Baada ya kumaiza kufanya installation, fungua application yako na taona category tofauti. Hapo utachagua Category na kuanza kuangalia bila tabu yoyote. (Zingatio: Ili kuweza kufurahia application hii ni lazima uwe na kifurushi cha data chenye MB za kutosha na mtandao wenye kasi nzuri kidogo).





Share:

Kazi zetu




 
 

                                                                                   


                                                                             




 HIZI PIA NI KAZI ZA TOPSERVICECARE

                                             

Share:

Mtandao Namba Moja Tanzania unaokuletea habari na mambo mengine yanayohusu teknolojia kwa ujumla kwa lugha ya Kiswahili!

Kiswahili ni Lugha Yetu!

Wasiliana nasi kwa maswali, nafasi ya kutangaza biashara yako au kupata huduma mbali mbali kama kunlock simu yako, Modem yako, Kwa huduma za flyers, Brochures , Computer maintanance , Calendar , Matangazo ya video kwaajiri ya biashara yako

Share:

Bei Nafuu

Huduma Ya Kunlock Modem Kwa Inapatikana kwa Bei nafuu
Tshs 5000
Share:

Unlock Simu Yako Leo

              Unlock Simu Yako Leo

HUAWEI ASCEND Y600, Y550, Y530 , Y330 , Y300, Y200, Y201,Y101,TiGO

 VODAFONE VF 685, V685, SMART KICKA, VodaCom


 VODAFONE V875 , V785 VodaCom


TECNO H6 TiGO.


 HUAWEI MOBILE Wi-Fi E5331 VodaCom, E5221 TiGO, ZTE R206z VodaCom


1.Je una simu au mobile wi-fi , wireless router , mi-fi yoyote kati ya hizo zilizotajwa hapo juu?
2. Je inatumia SIM CARD ya mtandao mmoja tu?
3. je unataka itumie mitandao yote bila kubagua?


Kama majibu yako ni ndio basi leo umepata suluhisho la matatizo yako

Basi leo umekutana na TOPSERVICECARE ambao ni wataalamu wa ku-unlock simu na vifaa vingine ili viweze kutumia mitandao yote. Tuna-unlock simu zote kwa kutumia unlock codes. Kwa wale wote wenye simu za HUAWEI na zinatumia line moja tu e.g. TiGO, au simu zote za VODAFONE zinazotumia line moja ya VodaCom tu basi wataweza kutumia mitandao yote yaani VodaCom, Airtel, TiGO, Zantel, TTCL, na mitandao yote duniani kote.
.

 NITAJUAJE KWAMBA SIMU YANGU INATUMIA MTANDAO MMOJA TU?
Utakapowasha simu yako ikiwa na SIM card tofauti itakutaka kuingiza namba moja wapo kati ya hizi zilizoorodheshwa hapa chini:-
---SIM network unlock pin
--- SIM service provider unlock pin
--- Network unlock code
-- Enter SIM Me Lock Code[NP]
-- Unlock Sim Block
-- Please Input Network Pin
-- SIM locked
--- SIM card locked! Please contact your operator! Reset Key?


QN1.NI TSH NGAPI HUDUMA HII?
Huduma hii ni sawa na bure kabisa. Ni Tsh 8000/= tu. Bei zetu hazina punguzo.

QN2.INAKUWAJE KAMA UNLOCK CODE NITAKAZOPEWA HAZITAFANYA KAZI?
Unlock code zinazotolewa ni "" FACTORY UNLOCK CODE"" , maana yake ni kwamba code hizi ni maalumu kwa simu husika tu na zinategema IMEI ya simu husika. IMEI inapatikana kwenye simu yako kwa kupiga *#06#.Hivyo basi unlock code kutoka TOPSERVICECARE kamwe haziwezi kushindwa kuifungua simu yako . Kila simu inakuwa na unlock code yake tofauti na zingine. Tangu tuanze huduma hii hakuna simu iliyowahi kushindikana hata moja.

QN3.JE KAMA NILIWAHI KUJARIBU KUINGIZA UNLOCK CODE ZA UONGO MPAKA SIMU IKAFUNGWA(BLOCKED) IKAANDIKA "UNLOCK SIM BLOCK" , JE NIFANYEJE?
kwa sasa hatuna huduma kwaambazo zimekuwa blocked.
 
QN4.JE SIMU ITAJIFUNGA TENA MTANDAO KWA SIKU ZIJAZO BAADA YA KU-UNLOCK AU NIKI-RESET SIMU?
HAPANA. Hata kama ukireset simu au ukiiformat au ukienda nayo nje ya nchi bado itaendelea kutumia mitandao yote duniani kote. Hii ndio maana ya unlocking.
Kwa wale watakaotaka kupata maelekezo ya ziada wanaweza wakawasiliana nasi kwa namba hiii ya simu ya mkononi..
VodaCom: 0757426730
Share:

Tangaza Nasi

Tangaza Nasi


TopServiceCare Team inatoa huduma kwa wanachi wote.


TopServiceCare Team inategemea Matangazo ilikujiendesha, Tunakaribisha matangazo ya ainazote. wasiliana nasi.

 Asante sana kwa mchango wako kwa kutangaza biashara yako  kwa kutumia
TopServiceCare.


TopServiceCare Mobile No : +255 757 426 730
Share:
Top Servicare. Powered by Blogger.

Web Design

Popular Posts

INSTAGRAM FEED

@soratemplates

Blog Archive

About