Monday, December 5, 2016

Tecno Camon C9 simu inayotikisa mjini kwa sasa na Camera kali ya Selfie

Kama wewe ni mtumiaji wa simu za Tecno tayari utakuwa unafahamu matoleo ya Camon ambayo lengo lake kuu ni kumuwezesha mtumiaji wa simu hizo kupiga picha nzuri na za kuvutia hata kwenye mwanga mdogo.

Tecno Camon C9 ipo tofauti kidogo kwani imekuja na teknolojia ya lens ya F 2.0 ambayo inawezesha mwanga mwingi zaidi kuingia katika kamera na kufanya picha ziwe na mwonekano mzuri zaidi huku ikiwa na Flash mbili ili kuongeza kiasi cha mwanga huo.

Tecno Camon C9 imepakiwa katika kasha zuri la rangi ya bluu na nyeusi ambalo kwa juu lina picha kama ya lens ambayo ni logo ya matoleo ya Camon.


c9-01


Nini utavikuta ndani ya Box?

  1. Simu ya Camon C9
  2. Chaja ya simu ya ukutani
  3. USB Cable
  4. Earpiece kwa ajili ya kusikilizia muziki
  5. Zana ya kutolea laini (SIM ejector tool)
  6. Flip Cover
  7. User manual, Warrant card na Palm chat Flyer
Simu hii inaumbo zuri linaloshikika kirahisi kiganjani na kwa upande wa nyuma ina umbo kama la yai.

Kamera na Flash

Hapa ndipo sifa ya simu hii inapokuja, ikiwa na kamera ya mbele yenye 13 MP iliyo katikati ya simu itamuwezesha mtumiaji hasa wapenzi wa selfie kupiga picha nzuri na bora zaidi. Uwepo wa kamera katikati ya simu kunaongeza uwezo wa mtumiaji kupiga picha za selfie za makundi kirahisi zaidi. Bila kusahau simu hii ina flash katika kamera ya mbele pia.

Kwa upande wa kamera ya nyuma C9 inakuja na kamera yenye uwezo sawa na ile ya mbele yaani 13MP huku ikiwa na double flash zilizozungushiwa ndani ya kiduara kuongeza uzuri zaidi.

Kava na Umbo

Kava la nyuma ni la plastiki ambalo linaweza kufunguliwa ili mtumiaji aweze kuweka laini na Memory kadi yenye uwezo mpaka wa 128GB. C9 imezungukwa na frame ya chuma na kuifanya simu kuwa ya hadhi tofauti na C8, C9 ina vitufe vyote upande mmoja wa simu na kumfanya mtumiaji aweze kuitumia kirahisi zaidi.

Simu hii inakuja na Flip Cover kwa ajili ya kulinda kioo chake, pale linapofunikwa kava hili linaweza kukibadilisha kioo cha simu hii kuwa kama saa ya analogia.

c9-05

Specifications za Simu C9

  • HiOS user interface based on Android 6.0 Marshmallow
  • Octa Core Processor
  • 16GB Rom 2GB Ram
  • 5.5″ FHD IPS Touchscreen (1080p)
  • 13 MP Front and Back Camera with Flashlight
  • Supports LTE Network (4G)
  • 3000 mAh Battery
c9-07

Bei (Shilingi 400,000/=)

Simu hii inapatikana maduka mengi ya jijini Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha kwa sasa kwa bei ya shilingi laki nne za kitanzania (400,000/=).


Share:

0 comments:

Post a Comment

Top Servicare. Powered by Blogger.

Web Design

Popular Posts

INSTAGRAM FEED

@soratemplates

Blog Archive

About