Nakusalimu ndugu na rafiki yangu!
“Jambo usillolijua ni sawa na usiku wa giza”. Huu ni msemo wa Kiswahili uliozoeleka miongoni mwa watu wengi. Nimeutumia kwa kuianza makala hii nikiwa na taswira ya kwamba watu wengi wana email na wengine wapo wengi tu hawana email wala hawajishughulishi kutafuta email. Lakini hata wale walionazo wengi wao hawajui namna ya kuzitumia ili ziwaletee faida kubwa. Wapo watu wachache ambao wameshagundua siri iliyopo kwenye email na kwa hiyo wameshachukua hatua mapema huenda hivi sasa wameshaanza kuvuna matunda yanayo patikana kwa kutumia email zao.
Mifano Halisi
Hapa Tanzania teknolojia ya kutumia mtandao kama biashara bado iko chini ukilinganisha na nchi zingine zilizoendelea. Kasi ya kutafuta taarifa au habari bado iko chini, watu wengi hawaelewi kuwa siri moja wapo ya kufanikiwa ni kutafuta taarifa. Kwenye kipindi kama cha uchaguzi au wakati wa ligi za mpira kidogo kasi ya kutafuta taarifa za aina fulani huwa inaongezeka hapa nchini,
lakini mara baada ya vipindi hivyo watu hupunguza kasi ya kutafuta taarifa, tofauti na nchi za wenzetu zilizoendelea ambapo kutafuta taarifa ni kazi ya kila siku katika maisha yao. Kwa sababu hiyo watu wengi wanatimiza ndoto zao. Kuwa na taarifa nyingi zilizo sahihi kwa wakati, kunakufanya upige hatua kubwa mbele mara nyingi kuliko watu wengine. Mtu asiye na taarifa huridhika na dhiki
yake na ikitokea siku moja kafanikiwa kupata kitu kikubwa kuliko wengine anaanza kujigamba eti yeye ni bora au tajiri au vyovyote vile. Hali hii mimi nimeishuhudia mara nyingi hasa kijijini. Mtu akijenga nyumba ya bati moja ya vyumba vitatu na sebure kila mtu kijijini hapo atamjua yeye ni nani. Utamkuta anajisifu mtaani na kwenye vilabu vya pombe. Majigambo haya ni kwa sababu
mtu huyu hana taarifa sahihi kwa wakati huo. Dunia iko mbali sana, usipokuwa na taarifa sahihi unaweza kujisifu kwenye kitu ambacho mbele ya wengine utaonekana hujui kitu. Lakini kumbuka kila hatua ya mafanikio unayofikia ni vizuri ukajipongeza ili iwe kama hamasa ya wewe kufanya vizuri zaidi wala usitake kufukuzana au kujilinganisha na mtu mwingine maana kufanya hivyo ni kupoteza muda.
Email Au Barua Pepe Inashika Kasi
Matumizi ya email yanaongezeka kwa kasi kubwa hapa duniani, watu wanatumia email zao kama njia ya kupata taarifa kutoka popote duniani. Kuna watu wengi wanajitolea kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao, mara nyingi wanatumia email kama njia ya kufikisha ujumbe wao kwa mtu binafsi.
Wajasiriamali wengi wanapenda kutumia email kwa sababu ni njia rahisi ya kufikisha mawazo yao na bidhaa zao za kijasiriamali kwenye jamii. Kutokana na mawasilano haya ya email mabilioni ya dola yanazunguka ulimwenguni mwote. Watu wengi waliojikita kwenye biashara ya mtandao hivi sasa ni matajiri
wakubwa. Mfano mzuri mitandao kama facebook, yahoo, google, twitter na makampuni makubwa kama goddady, amazon na mengine mengi yametajirika kwa njia ya biashara ya mtandao, lakini wote hao wanatumia email kama njia pekee ya kuwasiliana na wateja wao.
Baada Ya Kupata Wazo La Kutumia Email Kutimiza Ndoto Zangu, Kila Siku Nafaidika.
Tangu mwezi Septemba mwaka jana, 2014, nilipata kugundua kuwa kumbe email ni njia rahisi na ya haraka ya kupata mawazo mazuri ya mafanikio. Kuanzia hapo mpaka sasa nimejiunga na watu zaidi ya hamsini (50) kutoka kila
pembe ya dunia ambao hunitumia makala za aina mbalimbali kama vile makala za ujasiriamali, afya, mambo ya kiroho, ushauri wa biashara, vitabu, malezi ya familia na mengine mengi. Kwa siku huwa napokea wastani wa email za makala thelathini (30), ambazo kwa kiasi kikubwa zimenisaidia sana kufahamu wenzetu huko katika nchi zilizoendelea wanafanya nini!. Ninao watu wengi kutoka China,
Marekani, Tanzania, Afrika Kusini na nchi nyingine nyingi huwa wananitumia email zao zenye mafundisho ya huduma wanazozitoa kwenye maisha yao. Nafarijika sana ninapo “share” changamoto zangu na watu wengine hasa wale ambao wamejitoa kwa ajili ya kusaidia watu wengine wapate mafanikio.
Top Service Care Nimeianzisha Kwa Sababu Hiyo
Baada ya kuwa na marafiki wengi kiasi hicho wanaopenda ku-share changamoto zao na mimi kupitia email, nilipata kujiuliza sana kwanini watu hawa wananipenda kiasi hiki? Baada ya kutafakari sana, nikaamua na mimi kuanzisha huduma hii hapa Tanzania, ndipo nikafungua blog hii ya Top Service Care ambapo nimejitolea ku-share changamoto za maisha na wenzangu hasa
wale wanaopenda kupata mafanikio makubwa katika maisha yao. Mimi nimeshaweka msimamo wa maisha kwamba sitaki kusikia kitu kinachoitwa umasikini maishani mwangu. Wakati naanza safari hii ya kuelekea utajiri sipendi niende peke yangu nimeamua kubeba na wengine wengi wale walio tayari kusafiri pamoja na mimi kuelekea mafanikio makubwa. Kwa sababu hiyo
nakuandikia makala hizi zikusaidie pale unapokwama, lakini pia zikutie moyo pale unapokata tamaa ili hatimaye tuweze kufika wote kwenye raha ya mafanikio makubwa. Siandiki kwa ajili yako tu, bali ninapo andika na mimi napata kujifunza zaidi.
Unayo sababu Ya Kuitumia Email Yako Sasa
Kweli kabisa, anza kuitumia email yako kwa faida. Kitendo cha kuisoma hii makala maana yake bahati imekujia inataka ikuone unaamka na unaanza kufaidika kwa kutumia email yako. Jiunge na watu mbali mbali wanaotoa mafunzo au ushauri kwa njia ya email. Kila siku utapata mawazo mapya, kumbuka mawazo mapya ni msaada mkubwa sana kukusaidia kuvuka mahali
ulipo na hatimaye usonge mbele. Anza kwa KUJIUNGA na Top Service Care bure kwa email yako tu halafu kila siku ya jumatatu, jumatano na jumamosi utapokea makala nzuri ya kukusaidia na kukupa ushauri. Kama hiyo haitoshi kila mwezi utakuwa unatumiwa kitabu kimoja cha kukusaidia kwenye harakati zako za mafanikio yako. Hayo yote ni tisa, kumi utakuwa unajulishwa fursa
zinazopatikana hapa Tanzania au nje ya nchi kadri zinavyopatikana, halafu utakuwa unajulishwa kuhusu semina mbali mbali ndani na nje ya nchi, zote hizo utajulishwa kupitia email yako. Huu ni wakati wa kuchukua hatua sahihi, JIUNGE na TopServiceCare uanze kufaidi matunda hayo.
Kuna Fursa Nyingine Hapa Kupitia Email Yako
Unapojiunga kwa emil yako, mfano UKIJIUNGA na Top Service Care, utakuwa na uwezo wa kuuliza jambo lolote la kuhusu mafanikio kwa njia ya email halafu sisi hapa Morning Tanzania tutakujibu kwa ufasaha maana tuna wataalamu wa kila aina waliobobea kwenye sekta mbalimbali. Lakini pia kama kuna kitabu chochote unakitaka unaweza wasiliana na sisi kwa email: Topservicecare@gmail.com halafu tutakufatutia kitabu hicho.
Faida Nyingine Mbili (2) Unazozipata Kupitia Email Yako.
Kuwa na email yako na kuitumia ipasavyo kunakuwezesha kufanya mambo mengine mawili tofauti na niliyokueleza hapo juu.
Jambo la kwanza: Unaweza kununua kitu chochote kwa njia ya mtandao popote duniani. Nimekuwa nikinunua vitabu na vitu vingine kupitia email yangu. Na manunuzi hayo nalipia kwa malipo ya dola. Siku nyingine nitakuletea makala inayoelezea namna unavyoweza kununua kitu chochote kwa njia ya mtandao.
Jambo la pili: Email yako inakuunganisha na watu wengi wenye mawazo yanayofanana na wewe. Kupitia email yako unapata marafiki wengi ndani na nje ya nchi. Mfano, mimi nina marafiki wengi nje ya nchi na mmoja ameahidi kuja kunitembelea. Yote hayo unayapata kwa kuitumia email yako kwa lengo la kutimiza ndoto zako. Mimi nina ndoto za kutembelea nchi mbali mbali,
nitafanikisha hilo kwa kujipatia marafiki huko kupitia email yangu. Kama wewe unataka ubaki tu kijijini kwenu huko Mpalamawe, endelea kubaki huko, lakini mimi nataka kujifunza mengi na yote hayo nitayapata kupitia email yangu. Siongei haya ili nijisifu nakueleza ili uhamasike na uchukue hatua haraka na uweze kufaidika zaidi.
Kama huna smartphone, mimi nakushauri jikongoje ununue moja, nakushauri hivi kwa sababu ukiwa na smartphone utaweza kuzisoma email unazotumiwa
kwenye simu yako. Kwa hiyo hata kama uko mbali na kompyuta yako, bado utaweza kuzisoma email kwa urahisi zaidi. Nimekuwa nikizisoma email ninazotumiwa kwenye simu yangu, kwa hiyo hata nikiwa mbali na laptop bado naweza kufanya mambo mengi tu kwa kutumia smartphone yangu.
Nina Lingine Moja Hapa La Kuongezea
Maisha yako hakuna mtu mwingine atakaye yabadilisha. Usipochukua hatua wewe mwenyewe utabaki jinsi ulivyo maisha yako yote. Kwa wasichana nina
ushauri wa pekee, unatakiwa kufanya maamuzi mapema ya kuboresha maisha yako kabla hujaingia kwenye ndoa, maana ukiingia kwenye ndoa wakati mwingine unaweza kukosa uhuru. Ni heri ufanye maamuzi mapema. Biashara ya mtandao ni nzuri kama unaweza kuifanya anza sasa.
0 comments:
Post a Comment