Best File Manager Application
Bado ES File Explorer inaongoza katika orodha ya applications kali zaidi za kubrowse mafaili. Ikiwa na uwezo wa kuunganisha simu yako na laptop yako kupitia wifi, kucheza miziki na video za kwenye pc yako kupitia kwenye simu yako bila ya kuzisave, uwezo wa kumanage kila kitu katika vifaa vyako bila tabu yoyote ule kunaifanya ES Explorer kuwa App namba moja katika orodha hii.Ukiachana na ES File Explorer kuna Solid File Explorer ambayo kwa sasa inafanya vizuri na inakaribiana kila kitu na ES. Kwa kutumia Solid File Explorer utaweza kuweka vitu katika Dropbox, Drive au OneDrive moja kwa moja. Pia unaweza ukazip, RAR au kuhide mafolder katika simu au tablet yako.
Best Launcher Application
Unapozungumzia muonekano mzuri wa kioo cha simu yako kunaendana moja kwa moja na Launcher unayotumia. Mara nyingi watumiaji wengi wa Android hupendelea kuweka Launcher wanazozifurahia kila wanaposhika simu zao.Hapa ndipo Action Launcher 3 inapoingia. Ikiwa na interfae nyepesi na rahisi kutumia action launcher imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika orodha ya launcher za android.
0 comments:
Post a Comment